WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imefafanua
kuwa sifa ya kitaaluma ya waziri wa wizara hiyo ni Profesa Joyce
Ndalichako; na siyo Dk Joyce Ndalichako.
Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha wizara hiyo, ilisema tangu alipoteuliwa kushika wadhifa
huo wiki iliyopita, kwa bahati mbaya sifa ya kitaaluma ya waziri huyo,
imeendelea kujulikana kama Dokta.
“Tunapenda kuufahamisha umma kwamba cheo cha kitaaluma cha Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Dokta Joyce Ndalichako
kwa sasa ni Profesa Joyce Ndalichako”, ilisisitiza taarifa hiyo ya
wizara
Taarifa hiyo ilisema wafanyakazi wa wizara hiyo, wanampongeza waziri kwa
uteuzi huo na wanaahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu
yake kwa weledi na uadilifu katika kuendeleza sekta ya elimu na mafunzo
nchini.
0 comments :
Post a Comment