………………………………………
SERIKALI mkoa wa Arusha imefuta likizo zote za watumishi
ambao walikuwa wakitarajia kwenda mapumzikoni na kuwataka waendelee na
kazi kwa kushiriki kwenye mapambano ya kutokomeza ugonjwa wa kipindu
pindu ambacho kimeendelea kuwepo mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, maarufu kijiko,
ametoa maelezo hayo alipokuwa akiahirisha kikao cha kamati ya maafa ya
mko, na kusisitiza hakuna likizo mpaka kipindu pindu kitakapotokomezwa .
Amesisitiza Kwenye hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya
ya Arusha, Fadhili Nkurlu, mkuu wa mkoa amesema hadi Desemba 23 kuna
wagonjwa 14 ambao wamelazwa kwenye vituo mbalimbali na kusisitiza kuwa
Arusha bila kipindu pindu inawezekana hivyo watunishi na wananchi kwa
pamoja lazima kushirikiana ili kuondoa kabisa ugonjwa huo.
Ntibenda,amesema swala la kudhibiti ugonjwa huo linaonekana
kuachiwa idara ya afya pekee ambayo haiwezi kukabiliana na mlipuko wa
ugonjwa huo hivyo sewkta zote lazima kushirikiana kuutokomeza .
Akawawaomba viongozi wa kisiasa, kijamii, kimila kushiriki
kikamilifu kwenye mapambano hayo kwa kuwa ugonjwa wa kipindu pindu
hauna itikadi , hivyo akatoa wito kutolewa taarifa haraka pindi
kunapotokea mgonjwa au mwenye dalili za ugonjwa wa kipindu pindu .
Pia Ntibenda, akahimiza matumizi ya vyoo pamoja na
kuimarisha usafi wa mazingira ,sanjari na kuwachukulia hatua wale wote
watakaokuwa ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kusababisha kuendelea
kuwepo kwa ugonbjwa huo.


0 comments :
Post a Comment