HOSPITAL ya mkoa wa Arusha, Mount Meru,inakabiliwa na
upungufu mkubwa wa damu salama kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa
wanaohitaji damu kwa ajili ya matibabu yao.
Mganga mkuu wa hospital ya mkoa wa Arusha, Dakta Frida
Mokiti, amekiambia kikao cha kamati ya maafa ya mkoa wa Arusha, kuwa
hospital hiyo inahitaji uniti 1560 za damu salama,lakini akiba ya damu
salama iliyopo ni uniti 40 .
Kutokana na upungufu huo, mganga mkuu wa mkoa wa Arusha
Dakta Frida Mokiti, akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi
kujitolea damu nili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao matibabu yao
yanahitaji damu salama.
Amesema upungufu mkubwa wa adamu unasababisha wagonjwa
wanaosubiri matibabu yanayotegemea damu salama kuwa kwenye wakati
mugumu ili kuokoa maisha yao.
Dakta Mokiti, amewaambia wajumbe wa kikao hicho cha kamati
ya maafa ya mkoa kuwa makundi makubwa yenye uhitaji mkubwa wa damu
salama kwenye matibabu yao ni wajawazito, watoto na majeruhi .
Wajumbe wa kikao hicho ni pamoja na katibu tawala mkoa,
wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenye viti, madaktari wa wilaya na
mkoa,sekretarieti ya mkoa,na wataalamu wa ngazi mbalimbali na maafisa
afya .
Dakta Mokiti, amesema akiba ya damu salama iliyopo ni
kidogo sana kuokoa maisha ya wagonjwa ambao matibabu yao yanahitaji damu
nyingi,hivyo anaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa
maisha ya wagonjwa.
Dakta, Mokiti, amesema mahitaji makubwa ya damu salama
yanatokana na wingi wa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo hospital
kwa ajili ya matibabu yao,na pia hospital hiyo ya mkoa ndio inategemewa
na hospital zingine kupata damu.
Kwa upande wake kaimu katibu tawala wa mkoa huo, Anza
Amen Ndosa,aliwataka wakurugenzi wa haslmashauri za wilaya walifanyie
kazi na wasitumie bajeti kama visingizio ili kukwepa jukumu la kuchangia
damu salama kupita kwenye halmashauri zao.
Amesema uhai wa binadamu hautegeme bajeti bali damu hivyo
akazitaka halmashauri kuhamasisha wananchi kujitolea damu ili kuwezesha
kupatikana akiba ya damu salama ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao
matibabu yao yanategemea damu.
Nae mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu mkoa wa
Arusha,Dakta Christopher Nzela, amekiambia kikao hicho kuwa Msalaba
mwekundu,kimekuwa kikishiriki kuhamasisha wananchi kujitolea kuchangia
damu salama kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wanafikishwa
vhospitalini kwa matibabu .
Hamasa hiyo inayotolewa na msalaba mwekundu, imekuwa
ikisaidia kupatikana damu salama kutoka kwa wananchi wachache
wanaojitokeza kujitolea damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa.
Nzera, amesema mwamko mdogo wa wananchi imekuwa ni
changamnoto kubwa ya kufikia malengo ya upatikanaji wa damu salama na
hilo linatokana na kuwa na uelewa mdogo na kutokujiamini kiafya.
Inawezekana wananchi walio wengi hawana uelewa wa kujitolea
kuchngia damu salama,wengine hawajiamini hivyo wanakuwa na hofu ya damu
zao kukutwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi hivyo
inakuwa vigumu kujitolea kutoa damu.
Nzera, amesema msalaba mwekundu mkoani Arusha,imekuwa
ikihamasisha vijana wa shule za sekondari na vyuo ambao huwa wanakuwa
na mwamko mkubwa wa kujitolea damu salama,wakati makundi mengine ya
kijamii yakiwa hayashiriki.
Malawi yafanya ziara ya kujifunza katika sekta ya Habari na Mawasiliano
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Akisalimiana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack
Saidi alimpomtembelea ofisini kwake Leo Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Akisalimiana na
wageni toka Malawi walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es
salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Kushoto)
Alizungumza na ujumbe toka Malawi (Hawapo pichani) walipomtembelea ofisi
kwake leo Jijini Dar es salaam Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari
(MAELEZO) Assah Mwambene.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi akiwa na ujumbe
wake wakizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipomtembelea ofisi kwake leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mwenye shati la
batiki akizungumza na ujumbe toka Malawi walipomtembelea ofisini kwake
leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka
kushoto akizungumza na ugeni toka Malawi ofisi kwake leo kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack
Saidi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiagana na ujumbe
uliomtembelea toka Malawi leo ofisini kwake.
Mkurugenzi Idara ya Habari
(MAELEZO) Assah Mwambene akifafanua jambo kwa ujumbe uliotembelea Wizara
ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi.
Baadhi ya maofisa wakuu
walioambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka
Malawi wakifatilia mazungumzo yaliyofanyika Wizarani hapo Leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi akifaafnua jambo
kwa Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene walipokuwa
wakizungumza kwenye mkutano uliofanyoka leo Jijini Dare s salaam.
Mkurugenzi Msaidizi,sehemu ya
Usajili wa Magezeti toka Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo
Raphael Hokororo akifafanua jambo kwa ujumbe toka Malawi uliotembela
Wizarani hapo leo
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi (katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na ujumbe wake toka Malawi na na wakurugenzi wa
Habari toka Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kulia mwa
Katibu mkuu huyo ni Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
picha Na Raymond Mushumbusi MAELEZO


0 comments :
Post a Comment