Ligi
Daraja la Kwanza nchini (StarTimes First Division League) mzunguko wa
pili unaanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi katika viwanja tisa
mbalilimbali, huku michezo ya ligi hiyo
ikianza kuonyeshwa moja kwa moja
na kampuni ya Sahara Media kupitia kituo chake cha luninga cha StarTV.
Akiongea na waandishi wa habari
leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF, Meneja Masoko wa kampuni ya
StarTimes Tanzania, Damien Li amesema anashukuru michezo ya Ligi Daraja
la Kwanza inaanza kuonekana moja kwa moja kwenye luninga.
Damien alisema StarTimes
wanafarijika kuwa wadhamini wa kwanza kabisa wa ligi wa daraja la
kwanza nchini tangu kuanzishwa kwake, na sasa wanaviomba vilabu vyote
vinavoshiriki ligi hiyo kutumia nafasi hiyo kujitangaza ndani na nje
pamoja na wachezaji wao.
StarTimes ilingia udhamini wa Ligi
Daraja la Kwanza wenye thamani ya milioni 900 (mia tisa) za kitanzania
kwa kipindi cha miaka mitatu, huku kituo cha StarTV kikiongeza milioni
450 (mia nne hamsini) na kufanya udhamini huo kwa jumla kuwa ni bilioni
1.25 kwa kipindi cha miaka mitatu.
StarTv wataanza kuonyesha moja kwa
moja mchezo wa Jumamosi, Disemba 26 kati ya Friends Rangers dhidi ya
Polisi Dar mchezo utakaochezwa uwanja wa Karume, huku Jumapili Disemba
27 wakionyesha moja kwa moja mchezo kati ya Kiluvya United hidi ya
Ashanti United Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Naye Afisa Habari wa TFF, Baraka
Kizuguto, amevitaka vilabu vya Ligi Daraja la Kwanza kuitumia vizuri
nafasi hiyo kujitangaza kimataifa, kwa kuheshimu taratibu na kanuni
zinaondesha ligi hiyo.
Kizuguto amesema ligi hiyo itakuwa
ikirushwa moja kwa moja na kampuni ya Sahara Media kupitia kituo chake
cha StarTV, ambapo zaidi ya nchi 50 barani Afrika na Asia watapata
nafasi ya kushuhudia michezo hiyo.
0 comments :
Post a Comment