UFAFANUZI WA UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM HALMASHAURI YA WILAYA YA KYERWA

images (6)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa uamuzi wa mwisho kuhusu idadi ya Madiwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa kuwa ni Madiwani wanne kutoka Chama Cha Mapiduzi (CCM) na wanne kutokaChama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Tume imefikia uamuzi huu kufuatia malalamiko yaliyotolewa na CHADEMA, kwa nyakati tofauti
. Awali ilibainika kuwa Matokeo ya Udiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa yalikuwa na kasoro ambapo ilionyesha kuwa CCM walishinda kata 13 na CHADEMA walishinda kata 11 ambapo ukweli ni kuwa CCM walishinda kata 11 na CHADEMA walishinda kata 13.
 Pili,CHADEMA iliwasilisha malalamiko kuwa Tume imeibeba CCM kwa kuipa  Madiwani 5 wa viti maalumu na CHADEMA madiwani 4 wa viti maalum jambo ambalo lilisababishwa na kasoro ya matokeo ya Uchaguzi  wa Madiwani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupokea malalamiko hayo ilifuatilia kwa Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kyerwa ili kupata ufafanuzi kuhusu kasoro hizo za matokeo ya udiwani ambapo Msimamizi wa uchaguzi aliwasilisha matokeo sahihi ambayo yalionyesha kuwa CCM ilipata viti vya Kata 11 vya Udiwani na CHADEMA viti vya Kata 13, hatua ambayo ililazimu kufanya upya mgawanyo wa viti maalumu kwa kuzingatia kifungu cha 35(1) (c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 na  baada ya marekebisho hayo Tume ilimtaarifu Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kyerwa kupitia barua yenye kumb Na.AB.74/141/01 ya tarehe 08 Desemba,2015  kuhusu marekebisho ya viti maalumu vya Udiwani wanawake na hivyo kufanya CCM kupata viti 4 na CHADEMA viti 4 na kufanya idadi  ya Madiwani wanawake wa Viti maalumu kuwa 8 badala ya 9 vya awali.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetaja majina ya madiwani wa viti Maalum katika Halmashauri ya Kyerwa  kama ifuatavyo:
Madiwani wa Viti Maalumu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
  1. Restuta Kokuberwa Kafupa,
  2. Hyasinta Tibatekeleza Katia,
  3. Hassanat Muzeiyana Chamani, na
  4. Devotha Mkamungu Byashora.
Madiwani wa viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni
  1. Devotha Nestory Ikambuza,
  2. Consolata Sebastian Kanyima,
  3. Joyleth Godwine Mutashaga na
  4. Theophila Kokwenda Theobard.
Marekebisho yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 08, Desemba, 2015 na kutumwa Halmashauri ya Kyerwa yanapaswa kuzingatiwa katika hatua nyingine zinazofuata katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
Imetolewa na
 Jaji Mst DAMI.AN Z. LUBUVA
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment