- @nkupamah blog
Rais jimbo linalotaka kujitenga la Catalonia Artur Mas, wakati wa kikao cha Bunge katika mji wa
Barcelona, Novemba 9, 2015.
Na RFI
Mahakama
ya Katiba nchi Uhispania imefuta Jumatano hii azimio la Bunge la
Catalonia, ambalo lilianzisha rasmi mchakato wa uhuru katika jimbo la
Catalonia, lakini serikali ya mkoa huo mara moja imefahamisha kuwa
uamuzi huo ni batili.
Azimio hili "linakiuka viwango vya kikatiba ambavyo vinawapa watu wa Uhispania uhuru wa taifa", Mahakama imesema.
Majaji
wamesisitiza kuwa Bunge Catalonia haliwezi "kujipa uhalali wa majukumu
ya sheria na siasa, hadi kujipa uwezo wa kukiuka utaratibu wa kikatiba".
Majaji
kumi na mbili wamechukua uamzi wao kwa "kauli moja", kiongozi wa
serikali ya kihafidhina Mariano Rajoy amesema, huku akijipongeza.
Uamuzi
huo unakuja zikisalia wiki tatu kabla ya uchaguzi wa wabunge na siku
moja kabla ya ufunguzi rasmi wa kampeni za uchaguzi (Alhamisi usiku wa
manane). Bw. Rajoy anawania muhula mwingine wa miaka minne na anadai
kuwa ni msimamzi wa "umoja usio kuwa na mwisho" wa Uhispania.(P.T)


0 comments :
Post a Comment