Taarifa Kwa Wananchi Wote Kuhusu Majina Sahihi Ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Wednesday, December 2, 2015

@nkupamah blog

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa (Pichani) anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au
Kassim M. Majaliwa.

Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.

Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment