Waziri wa Afya, maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la
kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD
Prof.Idris Mtulia
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi
wa maghala hayo ,kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto
ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya
serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo
Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa
Waziri
Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi
ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya
Afya)
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Afya , Maendeleoya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya
Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali
linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri huyo ameeleza hayo baada
ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu
wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji
mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali na hilo, waziri huyo wa
Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na
serikali kwaajili ya Hospitali, vituo vya Afya na zahanati kununua dawa
hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema,
huku akisistiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika hatua nyingine ameishauri
Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa
moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati
wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo
zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza
kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa
inazofikisha.
Waziri huyo ambaye alifuatana na
Katibu Mkuu wa Wizara yake na watendaji wengine alitembelea maghala ya
kuhifadhia dawa ya Makao Makuu, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na
kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine
ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye
vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na
kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa
hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha
kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli
alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani
mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia
0 comments :
Post a Comment