EXCLUSSIVE: NI KWELI KAYUMBA WA BSS 2015, KAMJENGEA NYUMBA BABA YAKE? FEDHA ZILIZO BAKI? KASEMA YOTE HAPA

Mshindi wa Bongo star search (BSS) 2015 Kayumba Juma ambaye alijishindia kitita cha shilingi milioni
hamsini za kitanzania (50,000,000) baada ya kuibuka mshindi dhidi ya  wenzake katika shindano hilo

kayumbaasosie-20160125-0002Itakumbukwa kuwa wakati wa uombaji kura katika mchakato wa kumpata mshindi wa BSS 2015, kila mshiriki alikuwa anaeleza endapo atakuwa mshindi wa BSS 2015 kitita cha fedha atazao pata atazifanyia nini na kila mtu alieleza mipango yake.

Kwa upande wa Kayumba Juma ambaye aliwaomba watanzania wamchague na kuahidi endapo atashinda kiasi cha fedha atazo pata atamjengea nyumba baba yake mzazi kwa kuwa maisha mazima wamekuwa wana hangaika mahali pa kuishi.

kayumbaasosie-20160125-0001

Nkupamah media ilimtafuta kayumba Juma kujua ni kweli fedha alipatiwa? ni kweli ametekeleza ahadi kwa baba yake? na fedha zilizo salia anazifanyia nini? na majibu yalikuwa kama ifuatavyo.

“Fedha zote nilipewa na kitu cha kwanza nimemjengea nyumba baba yangu katika eneo la chanika Dar es salaam, na muda wowote anaweza kuhamia”  alisema kayumba ingawa hakutaka kutaja imegharimu bei gani.

“Kiasi kingine cha fedha nimenunua usafiri (gari) ndogo ya kutembelea na sasa fedha yote naiwekeza kwenye kazi yangu ya muziki ambayo kwa sasa ndio biashara pekee ninayo ifanya”

IMG_5338_800_600

Hata hivyo kayumba ameidokeza mtembezi.com kuwa nyimbo yake ya kwanza inatarajiwa kuachiwa tarehe February 6 mwaka huu, na hivyo mashabiki wakae mkao wa kula.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment