SI UNAJUA MRISHO MPOTO KAANZISHA KIJIJI CHAKE? SASA HII NI HABARI MPYA KUTOKA HUKO

Msanii na mtunzi wa mashairi ya nyimbo za asili Tanzania Mrisho Mpoto maarufu “Mjomba” katika kufanikisha ndoto ya mradi wake wa “kutoka
shambani” ambao upo ndani ya kijiji alichonunua msanii huyo na kukuiita Kijiji cha “Mpoto” Mkuranga Mkoani Pwani tayari kijiji hicho kimezinduliwa na kipo tayari kwa makazi ya watu huku baadhi ya mahitaji mengine yakiendelea kutimizwa.

IMG-20160123-WA0036Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Mrisho Mpoto katika uzunduzi huo aliambatana na balozi wa Kuwait Nchini Tanzania ambapo balozi huyo alizundua mradi wa kisima cha maji kijijini humo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kijiji hicho kwa kuwa maji ndio hitaji muhimu kwa binadamu.IMG-20160123-WA0034Kwa mujibu wa mrisho mpoto balozi huyo amefurahishwa na mradi wa msanii huyo ambapo ameahidi kutoa ushirikiano ndani ya mwaka 1 kwa kuongeza ukubwa wa eneo kutoka hekali 50 zilizopo sasa hadi 1000 ili kuhakikisha kijiji hicho kinabeba watu wengi zaidi sambamba na matrekta ya kilimo, ujenzi wa madarasa ya kujifunzia nz mabweni.

mpotoHata hivyo Mpoto amesema kijiji hicho kitawahusu watu wote waliokata kata tamaa na wasanii kuanzia umri wa 18-25 kwa jinsia zote ambao wameshindwa kujua ni wapi wataanzia kuhakikisha anajipatia kipato chake binafsi na kuendeleza fani aliyonayo ambapo kazi kubwa kijijini hapo itakuwa ni kilimo na muziki na zingine itakuwa ni uchongaji wa sanamu.

Kwa mujibu wa meneja wa mradi huo hauhitaji malipo ya aina yoyote kwa mtu atakaye jiunga na mradi wa “kutoka shambani” Gloria Kazahura walikuwa wamepanga kuanza na vijana 100 ndani ya mwezi huu, lakini mpaka sasa wamepokea maombi zaidi ya 3000, na hivyo zoezi la kupokea vijana litafanyika rasmi mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu na utaratibu maalumu utatolewa muda ukifika.MpotoUsipitwe na chochote kutoka Nkupamah media jiunge nasi kupitia www.nkupamah14.blogspot.com ,facebooknkupamahelia@yahoo.com upate habari zote saa 24/ si ku7za wiki, Pia unaweza kujiunga nasi kupitia simu yako ya mkononi yenye internet kwa kuandika moja kwa moja katika browser yako Nkupamah media ukapata habari zote za mtandao wetu..


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment