MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam Rumanyika leo
Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa serikali
yaliyowasilishwa na kujadiliwa Jan11, 2015 katika mahakama hiyo.
Katika mapingamizi ya serikali
Wakili wa serikali kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa
serikali aliweka mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya
Kafulila David kwa madai kwamba;
1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
3. kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria.
Katika uamuzi wa MAHAKAMA,
Jaji Rumanyika amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na
utetezi wa Wakili wa Kafulila imeamua kuwa;
1. Hoja kwamba hati ya
mashtaka haina au haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza
na kuamua KESI hii haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio
sawa na maombi ya kawaida na zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015,
kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya
kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazima kutaja ukweli
ulio hayana.
2. Hoja kwamba mahakama haina
uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya
2015 kifungu112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na
kutangaza mshindi alochaguliwa na hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi
hilo.
3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi
la Kafulila la kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA
imelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi
hivyo halina sababu kuwepo.
Baada ya maelekezo na maelezo
hayo, Mahakama haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama
ilivyombwa na wakili wa serikali na badala yake Kesi itaendelea January
28, 2015.



0 comments :
Post a Comment