Wananchi wa Kata ya Usagara,
wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya
Gulio mjini Usagara. Wananchi hao
walimwambia Waziri Kitwanga
wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge
huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais
mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji
yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Picha zote na Felix Mwagara.
Kikundi cha Burudani kinachoitwa
Mawe Matatu cha Kata ya Usagara, wilayani Misungwi kikitoa burudani
kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) kuzungumza
na wananchi wa kata hiyo katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Katika
hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua na
pia atahakikisha kero zote anazitatua. Hata hivyo, wananchi
hao,walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli
wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la
maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao
ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara kuhusu masuala
mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lake. Kitwanga aliwataka wananchi hao
washirikiane katika kuchangia miradi ya maendeleo ili jimbo hilo liweze
kupata mafanikio zaidi. Hata hivyo, wananchi hao walimuambia Waziri
Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi
Mbunge huyo kipindi cha kampeni, alisema suala la maji atalishughulikia
Rais mwenyewe, hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili
maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Hata hivyo maandalizi ya
upatikanaji maji zimeanza jimboni humo.
Msimamizi wa Mradi wa Maji
Mwanza, Abbas Muslim akijibu maswali ya wananchi baada ya Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi,
Charles Kitwanga (kulia) kumtaka ajibu maswali ya wananchi hao kuhusu
lini maji yatapatikana jimboni humo pamoja na hatua walizozifikia mpaka
sasa. Hata hivyo, Msimamizi huyo alitoa ufafanuazi kuhusu mradi huo na
kuwafafanulia wananchi hao kuwa, mradi huo mkubwa wa maji unaojumuisha
Misungwi, Magu, Lamadi, Musoma, Bukoba na Jiji la Mwanza unatarajiwa
kumalizika mwaka 2018 lakini pia unaweza ukamalizika kabla ya muda huo
uliopangwa na wananchi kuweza kupata maji. Picha zote na Felix Mwagara.


0 comments :
Post a Comment