Mwenyekiti wa Kamati ya
kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari(hawapo
pichani) leo jijini Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya
kuratibu Miss Tanzania ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino
International Agency, kushoto ni Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo
na kulia ni Mjumbe wa kamati Gladys Shao .
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu
Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili
mfumo ili kubadilisha muonekano wa mashindano ya urembo(Miss Tanzania)
kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa
Kamati ya kuratibu mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo
pichani) alipokuwa akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano
hayo.
PICHA NA Beatrice Lyimo-Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………….
Lilian Lundo- Maelezo
Dar es Salaam.
Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.
“Tumekuja
kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino
International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya
Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya
kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.
Pinto aliongeza kwa kusema kuwa
kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika
kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino
imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.
Kamati hiyo imefanya vikao
vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili
kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino
ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.
Kutokana na kutopata muafaka
katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya
kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua
kujitoa katika Mashindano hayo.
Aidha, Pinto amewaomba radhi
wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya
kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino
kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.
0 comments :
Post a Comment