Mkuu wa Mizani Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), Eng.Lucian Kilewo akifafanua jambo katika mafunzo
ya kuwajengea uelewa wa pamoja maafisa uendeshaji wa Mizani
yanayofanyika mjini Morogoro.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa
matengenezo wa
TANROARDS Eng.Joseph Lwiza akifuatiwa na Mkurugenzi wa
Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng.Julius Chambo na Kaimu Mkurugenzi msaidizi Eng.Joyce Mbunju.
Maofisa uendeshaji mizani nchini wakifuatilia mada katika mafunzo ya kujengewa uelewa wa pamoja mjini Morogoro.
………………………………………………………………………………………………
Wafanyakazi wa Mizani hapa nchini
wametakiwa kufanya kazi kwa uwazi, uadilifu, na weledi ili kuzingatia
sheria zinazoongoza sekta hiyo na hivyo kutenda haki kwa wasafirishaji
wote na kujenga taswira nzuri kwa taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng.
Julias Chambo katika mafunzo kwa maofisa waendesha mizani hapa nchini
yanayofanyika mjini Morogoro.
“Sasa tubadilike tujenge taswira
njema katika sekta ya mizani kwa kuepuka vitendo vya rushwa kwa kufanya
kazi kwa uwazi na kulinda barabara zetu”, amesema Eng. Chambo.
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea
uelewa wa pamoja watumishi wote wa mizani nchini juu ya utelekelezaji
wa majukumu yao na kupunguza malalamiko yasio na msingi katika sekta
hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi.
Naye mkuu wa mizani wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS), Eng Lucian Kilewo amewataka watumishi wa
mizani kutumia elimu walioipata katika kutekeleza majukumu yao na
kuipeleka kwa wenzao ili sekta hiyo ipate mabadiliko yanayoendana na
wakati wa sasa.
“Mafunzo haya yataendelea mara
kwa mara ili kuhakikisha mnakuwa na uelewa wa pamoja katika kuimarisha
sekta ya mizani nchini na kuiwezesha kufanyakazi kwa tija na kulinda
barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi”. amefafanua Eng. Kilewo.
Mkurugenzi wa matengenezo
(TANROADS) Eng. Joseph Lwiza amesema Wakala wa Barabara nchini
wamejipanga kutatua changamoto zinazojitokeza katika vituo vya mizani
nchini kote na kuwa na mfumo mmoja utakaowezesha kazi zinazofanywa
katika mizani kuonekana moja kwa moja makao makuu ya TANROADS na
Wizarani ili kuimarisha uwazi na kudhibiti rushwa.
Wataalam hao wa mizani pia wametembelea mizani zinanopima uzito wa magari katika mwendo weigh in motion katika eneo la Mikese na Vigwaza na kujionea mfumo huo unavyofanya kazi na kupunguza msongamano wa magari.
Takriban mizani 70 zinapima uzito
wa magari hapa nchini tatu zikiwa za magari yanayopimwa yakiwa katika
mwendo, 29 mizani za kuhamisha-mobile na 41 mizani za kudumu –fixed ambapo nia yake ni kuhakikisha magari yababeba uzito unaokubalika ili kulinda barabara.
0 comments :
Post a Comment