Waislamu wa madhehebu ya Shia wameandamana maeneo mengi kushutumu mauaji ya Sheikh al-Nimr
Kuwait
imetangaza kwamba inamuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu
kuuawa kwa
mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi.
Ubalozi
wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji
waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh
Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata.
Marekani, UN na Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizohimiza kuwepo kwa utulivu Mashariki ya Kati.
Saudi Arabia na Iran ndizo nchi kuu za Kisuni na Kishia mtawalia eneo la Mashariki ya Kati na zimekuwa wapinzani wakuu.
Nchi hizo huunga mkono pande pinzani katika mizozo Syria na Yemen.
0 comments :
Post a Comment