Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeipongeza Manispaa ya Ilala kwa kutoa huduma bora za afya kwa wanachama wa mfuko huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, katika ufunguzi wa mkutano wa watoa huduma wa
afya uliofanyika
leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
salaam,Mkurugenzi wa Masoko,Elimu kwa Umma na Utafiti Othuman Rehani amesema kwamba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatambua mchango mkubwa unaotolewa na watoa huduma za afya kwa wanachama wao.
“Utoaji wetu wa huduma za afya za kijamii kwa wanachama wetu umekua ukitegemea Hospitali za Umma na Binafsi”alisema Rehani.
Mkurugenzi
Othuman Rehani aliongeza kuwa NHIF wanaamini kwamba, ushirikiano na
watoa huduma utasaidia Serikali yetu ya awamu ya tano kufikia lengo lake
la kutoa huduma bora.
Aidha
Rehani ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa
Bima ya Afya mwaka 2001 yakiwemo; kupanuka kwa upatikanaji wa huduma kwa
kuongezeka kwa vituo vya kutolea tiba vilivyosajiliwa na mfuko,usajili
wa maduka ya dawa yalioongeza upatikanaji wa dawa hadi vijijini,utoaji
wa mikopo ya madawa na vifaa tiba ili kuimarisha utoaji wa huduma za
afya pia kuongezwa kwa vitita vya mafao kwa wanufaika waliokua
wakiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika
mkutano huo wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria ni pamoja na Mganga
Mkuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Meneja
Mfawidhi wa Mkoa wa Ilala na Wakurugenzi wa Hospital za Rufaa.
Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya umetimiza miaka 14 toka ulipoanzishwa na kuanza
utekelezaji wake mwaka 2001 ikiwa na watoa huduma za afya wale wa
hospitali za Umma na Binafsi waliokamilisha usajili wao katika Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Wazee na Watoto.(P.T)
0 comments :
Post a Comment