Mchezaji Mbwana Samatta
aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ndani
nchini Nigeria akimkabidhi jezi yake Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makzi Mh. Wiliam Lukuvi katika hafla iliyofanyika
kwenye
hoteli ya Hyyat Regency jiji Dar es salaam usiku huu.
Baadhi ya wanamichezo
waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajiri ya Simba Bw. Zakaria Hanspope, Saleh ali Mhariri wa Gazeti la
michezo la Champion na Wakili wa Vilabu shiriki vya Ligi kuu Tanzania
Bara mwanasheria Damas Ndumbalo wakibadilisha na mawazo katika hafla
hiyo
Mchezaji Mbwana Samatta
aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ndani
nchini Nigeria amezawadiwa na serikali kiwanja kilichpo Kigamboni jijini
Dar es salaam na fedha taslimu ambazo kiasi chake hakijafahamika hayo
yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi Mh. Wiliam
Lukuvi anayeonekana katika picha katika hafla iliyofanyika kwenye
hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi
kadhaa wa serikali.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria
katika hafla hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.
Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel
na viongozi wengine wengi wa serikali na wanamichezo.
Mbwana Samatta aliyekuwa
akicheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo inayomilikiwa na tajiri wa madini na aliyewahi
kuwa Gavana wa jimbo la Katanga nchini humo Moise Katumbi anatarajiwa kujiunga na timu ya KRC Genki ya Belgium barani ulaya, Hafla hiyo imefanyika usiku huu jijini Dar es salaam.


0 comments :
Post a Comment