UNANAJUA WAZIRI MBARAWA AMEWATAKA MAKANDARASI KUFANYA NINI ? Soma Habari Hii..........

Nkupamah Media:

Mkandarasi wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami

mba2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
mba3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
mba4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
mba5
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.
mba6
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
mba7
Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
…………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.
Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.
“Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.
Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.
“Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.
“Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.
Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu  kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.
Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2  na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment