Virusi vya Zika:Waonywa kutoshika mimba Brazil

  • Dakika moja iliyopita Watoto walioathirika na Zika
Maafisa wa Afya wa Brazil wanasema kuwa wanahofia kwamba maradhi yanayoenezwa na mbu ya
virusi vya Zika huenda yameenea kuliko walivyotarajia.
Virusi hivyo vimedaiwa kusababisha ongezeko la ulemavu miongoni mwa watoto wadogo wanaozaliwa nchini humo.
Hofu imetanda wakati huu ambapo mji mkuu wa Rio unatarajia kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympiki mwaka huu.

IKukabiliana na virusi vya Zika
Watafiti wamesema kuwa hali ya hewa yenye unyevu mkubwa ndiyo iliyochangia pakubwa mlipuko wa maradhi hayo.
Kampeni ya kuwahamasisha wananchi kuyaondoa maji yaliyosimama, ambako mbu wanazaana imeanzishwa huku juhudi za kubuni chanjo zikiendelea.
Idara ya Afya nchini Marekani imewaonya wanawake waja wazito wasitembelee mataifa 20 katika eneo la Brazil, kukiwemo sehemu zingine kama vile visiwa vya Samoa na Cape Verde.
 Mbu wanaosababisha ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba karibu mataifa kumi ya Afrika, Asia na Pacific pia yametangaza mlipuko wa maradhi hayo ya Zika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment