YANGA YACHEZESHEWA KICHAPO CHA MBWA MWIZI.... KUTOKA MKWAKWANI: COASTAL UNION 2-0 YANGA (FULL TIME)

Nkupamah media:


KADI Dk 90+9 Yondani naye analambwa kadi nyekundu na kwenda moja kwa moja vyumbani  KADI Dk 90+9, daktari wa Coastal aliyeingia kumtibu kipa, analambwa kadi nyekundu DK 90+5 Mwamuzi anatoa kadi nyekundu halafu anairudisha  DK 90+4 Yanga wanapata kona, shambulizi kali, Ngoma anapiga kichwa, lakini walinzi wa Coastal wako ngangari kwelikweli 
DAKIKA 7 ZA NYONGEZA

Dk 88, Paul Nonga anapiga shuti kali na mpira unagonga mwamba, Coastal wako vizuri wanaondosha mpira
 Dk 86, Yanga wanapata kona, Msuva anaichonga, shambulizi ni kali lakini hakuna kitu DK 81 hadi 83, Coastal wanaendelea kuonekana wako vizuri kwa kucheza kwa juhudi ya juu kabisa Dk 79, pasi nzuri ya Joshua, Nonga anaiwahi lakini mpira unawahiwa vizuri na kipaSUB Dk 74, Yanga wanamuingiza Paul Nonga ili kuongeza nguvu Dk 69, Tambwe na Ngoma wanapoteza mpira, wanashindwa kufunga wakiwa peke yao baada ya krosi nzuri ya Juma Abdul 
GOOOOOOOOO Dk 62, Juma Mahadhi, kijana aliyekuzwa na Jackson Mayanja anafunga bao safi kwa shuti kali, Coastal 2, Yanga hawajapata kitu 
Dk 54 hadi 59, bado inaonekana mpira umepoteza ladha, nguvu zaidi inatumika zaidi na Coastal kidogo wanakuwa na kasi katika ukabaji 
Dk 50 hadi 53, mpira unaonekana kupoteza malengo hasa kiuchezaji na zaidi unachezwa juu au kubutua Dk 46 hadi 49, Yanga wanaanza kwa kasi wakionyesha wamepania kusawasisha. Lakini Coastal wanaonekana hawana hofu 
MAPUMZIKO Dk 45, Coastal wanacheza taratibu wakionyesha kupania kuumiliki mpira taratibu huku Yanga wakionyesha kuwa na prsha kubwa 
KADI Dk 44, Chidiebere analambwa kadi ya njano kwa kutembeza ubabe kila mara Dk 37, Msuva anapiga krosi ya juu ambayo inakosa mwenyewe na kuwa goal kick 
Dk 34, Coastal Union wanaonekana kurudi nyuma ili kuongeza ulinzi wa bao lao hilo moja wanalotaka kumaliza nalo dakika zote 45 Dk 32, Yanga wanapata kona inachongwa na Msuva, mpira unamfikia Ngoma anapiga shuti kali, mwamuzi anasema ni offside 
KADI Dk 30, Twite analambwa kadi ya njano kwa kufanya ubabe GOOOOOO Dk 27, Miraji Adamu anaifungia Coastal Union bao kwa mkwaju wa adhabu baada ya Yondani kuunawa mpira. Alipiga faulo, mpira ukamshinda Dida ambaye anafungwa bao baada ya mechi saba kucheza bila ya kufungwa 
Dk 23, Juma Mahadhi anapiga shuti kali kabisa lakini linatoka nje kidogo. Ilikuwa ni baada ya shambulizi kali zaidi la Coastal 
 
Dk 18, Ngoma anaruka na kupiga kichwa hatari kabisa, lakini kipa anafanya kazi nzuri kabisa na kuokoa 
Dk 17 KADI Sabo Yusuf wa Coastal analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Kamusoko Dk 12 hadi 13 zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na mashuti ya mbali huku hakuna anayelenga lango 
Dk 11, Twite anatolewa kwenda kutibiwa nje baada ya kukanyagwa kwa makusudi na Shiboli Dk 8, shambulizi la kwanza la Coastal Union, Miraj Adam anapiga mkwaju mzuri wa adhabu, lakini anapaisha 
Dk 7, pasi nzuri kabisa ya kamusoko, Tambwe anachelewa na Coastal na kuokoa.
Dk 4, Miraj Adam anaruka na kuokoa mpira wa krosi ya Msuva, inakuwa kona, inapigwa na Msuva, lakini haina madhara 
Dk 2, Yanga wanapata kona, inachongwa na Simon Msuva, lakini Bakari, kipa kinda wa Coastal, anaruka na kudaka vizuri kabisa
Dk 1, mechi inaanza taratibu sana huku kila timu ikionekana kuwa makini



KIKOSI KAMILI...

1. Deogratias Munishi-30
2. Juma Abdul-12
3.Oscar Joshua-3
4. Kelvin Yondani-5
5. Vicent Bossou-9
6. Mbuyu Twitwe-6
7. Simon Msuva-27
8.Thabani Kamusoko-13
9. Amissi Tambwe-17
10. Donald Ngoma-11
11. Deus Kaseke-4

BENCHINI:
Gk Ally Mustafa-1
2. Pato Ngonyani-15
3. Said Juma-22
4. Matheo Antony-10
5. Paul Nonga-26
6. Salum Telela-2
7. Issofou Boubacar-14

KOCHA MKUU Hans van der Pluijm
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment