Nkupamah media:
MKurugenzi wa kampuni ya Advanced
Security Company Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akimtambulisha
bondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) mbele ya bondia Geard Ajetovic
(wa kwanza kushoto) huku promota Jay Msangi (wa pili kushoto)
akishuhudia.
Promota Jay Msangi (katikati) akiutambulisha mkanda kwa mabondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) na Geard Ajetovic (kushoto)
Bondia Francis Cheka (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Geard Ajetovic mara baada ya kukutana mara ya kwanza.
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Bondia nyota wa ngumi za kulipwa
nchini, Francis “SMG” Cheka amesema kuwa Mserbia anayeishi Uingereza,
Geard Ajetovic atampa kipigo ambacho hata kisahau katika maisha yake
katika pambano lao lililopangwa kufanyika Jumamosi, kwenye viwanja vya
Leaders Club
Cheka alisema hayo walipokutana
kwa mara ya kwanza katika mkutano na waandishi wa habari iliofanyika
kwenye ukumbi wa Sinema wa Mlimani City jijini.
Alisema kuwa Ajetovic amekosea
kukubali kupambana nay eye katika ardhi ya Tanzania kwani mwaka 2008
alishindwa kwa pointi kutokana na maamuzi ya majaji ambao
walimpendelea.
“Nimejiandaa vilivyo kwa ajili ya
pambano hili,nilikuwa Zambia nilikfanya mazoezi ya wiki mbili, huyu
jamaa ananiita mimi babu wakati wote tumezaliwa miaka ya 1980, atajuta
nakuambia, amenizalilisha sana nami nitamjibu ukumbini,” alisema Cheka.
Wakati huo huo; Mkanda wa ubingwa
wa mabara wa WBF utakaogombewa na mabondia Francis Cheka na Muingereza,
Geard Ajetovic umewasili nchini.
Mapema rais wa WBF, Goldberg
Haward na marefarii kutoka Afrika Kusini waliwasili jijini Dar es Salaam
wakiwa na mkanda huo utakaogombewa na mabondia hao kesho kwenye viwanja
vya Leaders.
Muda mfupi baada ya mkanda huo
kutua nchini, Cheka na Ajetovic walipata fursa ya kupiga nao picha
wakiwa sanjari na makocha wao, Abdallah Salehe ‘Comando’ na Aksu
Sahhaydar.
Kwa nyakati tofauti jana,
mabondia wote wawili walitambiana huku Cheka akibainisha kutotishwa na
tambo za mpinzani wake huyo ambaye aliwasili nchini Jumanne iliyopita
akitokea Ujerumani alikokuwa ameweka kambi.
“Siku zote naamini maneno si
vitendo, sitaki kuzungumza mengi lakini nitazungumza ulingoni Jumamosi,
nimesikia tambo za mpinzani wangu lakini nasisitiza tena, sijawahi
kuwaangusha Watanzania nchini kwetu na sitarajii iwe hivyo Jumamosi, cha
msingi ni wao kunisapotio siku hiyo,” alisema Cheka.
Mkurugenzi wa Advance Security,
Juma Ndambile alisema mabondia hao watapima uzito na afya Alhamis saa
tano asubuhi kwenye hoteli ya Palm Beach tayari kupanda ulingoni hapo
kesho.
“Kila kitu kimekamilika,
kiingilio VIP itakuwa elfu 50 na viti vya kawaida ni Sh elfu 15, milango
ya Leaders itakuwa wazi kuanzia saa nane mchana ambapo kutakuwa na
burudani mbalimbali ikiwamo ya bendi ya Twanga Pepeta kabla ya mapambano
kuanza saa moja usiku yakitanguliwa na mapambano ya utangulizi.
0 comments :
Post a Comment