Ndoto ya muda mrefu ya mashabiki wa Manchester United kumuona kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho akifundisha klabu yao inaonekana kukaribia kutimia baada ya kuwepo kwa taarifa za Mourinho kujiunga na Man United.
Kwa mujibu wa mtandao wa Dailymail umeeleza kuwa Mourinho amewaambia marafiki zake kuwa atajiunga na Man United baada ya kumalizika kwa msimuu huu wa 2015/2016.
Taarifa za Mourinho kujiunga na Man United zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali licha ya kocha wa sasa wa Man United, Louis Van Gaal kukanusha na kueleza kuwa atasalia kwenye klabu hiyo.
Jose Mourinho (kulia) akisalimiana na kocha wa sasa wa Manchester United, Louis Van Gaal kipindi akiwa bado ni meneja wa Chelsea
Aidha siku kadhaa zilizopita Mourinho alieleza kuwa anataraji kurejea katika kazi muda wowote kwa siku za karibuni licha ya kukataa kuitaja klabu ambayo atakwenda kuifundisha.



0 comments :
Post a Comment