Msanii wa muziki Nuh Mziwanda, hatimaye ameamua na yeye kufuta tatoo ya Shilole aliyokuwa ameichora mkononi, akienda tofauti na nadhiri aliyojiwekea ya kwenda kaburini na tatoo hiyo.
Nuh amesema kuwa, ameamua kufanya hivyo alipogundua tabia halisi za Shilole baada ya kuachana naye, akidai kuwa ex wake huyo ameingilia ukurasa wake wa instagram (hacking), akimtukana katika mahojiano mbalimbali, kitu ambacho kimemfanya kugundua kuwa msanii huyo alikua si rafiki yake.
Nuh mbali na kuchora tatoo mpya juu ya ile ya Shishi Baby, ameongeza tatoo nyingine kadhaa mwilini kwake, ikiwepo usoni kama ambavyo inaonekana katika picha.
0 comments :
Post a Comment