Mamluki Waliobaki Ndani ya CCM Siku zao Zinahesabika..Jakaya Kikwete Aagiza Waanze Kushughulikiwa



MAMLUKI waliobaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku zao zinahesabika, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, kumuagiza Makamu Mwenyekiti, Tanzania Bara, Philip Mangula kuanza kuwashughulikia.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Namfua, mkoani Singida, Kikwete alisema chama hicho kimevuka salama katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa Oktoba mwaka jana, pamoja na baadhi ya wenzao kuondoka.

“Tunashukuru uchaguzi ulipita na Chama kimevuka salama katika mchakato mzito kinyume na watu walivyotutabiria kifo… haukuwa rahisi kwetu kwa sababu ulizidiwa na kelele na vitisho pamoja na kuwepo wenzetu waliotuhama na kudhani tutakufa lakini hatukutetereka.

“Tunajua wako wengine waliobaki kama mamluki, lakini wajue siku zao zinahesabika maana hatutakubali kuendelea kunyonywa damu, natumaini Mangula umeanza kuwashughulikia hawa mamluki,” alisema Mwenyekiti huyo anayemaliza muda wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment