Nkupamah Media:
Jana Mbwana Samatta alipata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha KRC Genk ambayo inashiriki ligi kuu ya Ubelgiji iliyomsajili hivi karibuni kutoka klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Nahodha huyo mpya wa Stars aliingia uwanjani dakika ya 73 kipindi cha pili wakati timu yake tayari ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi ya nchini humo.
Genk itashuka dimbani Jumamosi ijayo February 13, dhidi ya Waasland kwenye uwanja wa Cristal Arena ambao ndiyo uwanja wa nyumbani wa Genk. Mechi hiyo itachezwa saa 4:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments :
Post a Comment