Nkupamah media on Sunday, February 28, 2016
Askari
polisi mjini Iringa akiwa ameshika kisu baada ya kufanikiwa kumnasa
kijana Mohamed Iddy (18) mkazi wa mjini Iringa kutokana na kutishia
maisha ya wakazi wa mji wa Iringa akiwa katika shughuli yake ya
kuomba hudaiwa kuhatarisha maisha ya wananchi kwa kuwafukuza kwa kisu
pindi anaponyimwa pesa ,
Kijana
huyo omba omba tishio akipelekwa kituo cha polisi pamoja na kisu
anachotumia kutishia wananchi wakati akiomba pesa
Askari polisi wakiwa wamembana vilivyo kijana huyo omba omba
Hapa akiwa eneo la Miyomboni akipelekwa kituoni
OMBA
omba hatari anayeomba kwa nguvu kwa kutumia kisu kwa wananchi
wanaomnyima msaada wa pesa amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa
Iringa kufuatia msako mkali dhidi yake.
Tukio la kukamatwa kwa kijana huyo lilitokea leo majira ya saa 5
asubuhi katika eneo la Posta mjini Iringa baada ya kuwepo kwa
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa mji wa Iringa hasa wanawake
ambao wamekuwa wakifukuzwa kwa kisu na kijana huyo omba omba baada ya
kumnyima pesa.
Mmoja kati ya wanawake ambao wamepata kutishiwa kuchomwa kisu na
kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Mohamed Iddy Chengula (18) Bi Amina
Said mkazi wa Mkwawa alisema kuwa ni zaidi ya mara mbili
amenusurika kuchomwa kisu na kijana huyo omba omba .
Alisema kuwa mji wa Iringa una omba omba wengi ila mbinu hiyo
anayotumia kijana Mohamed ya kutembea na kisu na kuomba kwa kutishia
kisu ni mpya kutokea mjini hapa na ni omba omba pekee ambae kwa
mwonekano haonyeshi kama ni omba omba anaonyesha ni kijana mtanashati
mzuri ila vitendo vyake ndivyo vimekuwa tishio kubwa kwa wananchi.
Huku vijana wauza
magazeti eneo la Posta walidai kuwa ni mara kadhaa wamekuwa
wakishuhudia mbinu chafu za kijana huyo ambazo wao wanafananisha
na unyang'anyi na sio omba omba wa kawaida .
Kwani walisema
haiwezekani kama ni omba omba kweli kutembea na kisu na pindi
anaponyimwa pesa anachomoa kisu na kutaka kumchoma yule aliyemnyima
pesa na wakati mwingine huwafukuza hasa wanawake .
Vijana hao walisema
tukuo la leo kwa omba omba huyo kutishia kumchoma mtu kisu mbele
ya askari hao ndilo ambalo limefanikisha kukamatwa kwake .
Hata hivyo askari
hao walionyesha ukomavu mkubwa wa kiaskari katika kumkamata ombaomba
huyo ambae alikuwa akitishia kuwachoma kisu kabla ya kumdhibiti
kisawa sawa na kumpeleka kituo cha polisi.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Peter Kakamba pamoja na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo
alitaka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi
wanapoona matukio ya watu kama hao kwani ni hatari katika jamii
0 comments :
Post a Comment