Nkupamah media:
Ziara
ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga
Mpina, ziarani katika baadhi wa viwanda jijini Arusha. (Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais).
kikao kikiendelea.
Naibu
waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina amekiamuru
kulipa faini kiwanda cha A to Z cha mjini Arusha , chenye kufanya kazi
ya kuzalisha nguo na bidhaa za plastiki kutokana na ukiukwaji wa
utekelezaji wa sheria namba 20 ya mwaka 2004 ya utekelezaji na usimamizi
wa mazingira.
Mh
Mpina alitoa agizo hilo jijini Arusha Jumamosi katika ziara yake ya
kukagua usafi wa mazingira, kupanda miti na kutembelea viwanda,ambapo
alibaini kuwa mnamo septemba mwaka 2015 kiwanda hicho kilipewa adhabu ya
kulipa faini ya shilingi milionni 70 na kukaidi kufanya hivyo kwa
kipindi cha miezi sita sasa.
Mh
Mpina amekitaka kiwanda hicho kulipa faini hiyo kwa kipindi
kisichopungua siku saba kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa.Aidha
Naibu Waziri Mpina alitembelea viwanda vya Sunflug na Lothia Steel vya
jijini humo na kujione namna ambavyo vinakabiliana na utunzaji wa
mazingira katika uzalishaji wao na changamoto ya kuzimikazimika kwa
umeme jijini Arusha.
Mh.
Mpina alikitaka kiwanda cha Chuma cha Lothra Steel kupima moshi
unaotoka katika kiwanda hicho ili kujua kama una athari kwa mazingira na
viumbe vinavyozunguka maeneo ya kiwanda hicho.Ziara na Mh waziri katika
jiji la Arusha ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Mh Rais John Pombe
Magufuli la usafi wa mazingira unaotakiwa kufanyika kitaifa kila
Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
0 comments :
Post a Comment