Panga Pangua Ya Rais Magufuli Imemgusa Bi. Suzan Paul Mlawi Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria

Nkupamah Media:


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemhamisha Bi. Suzan Paul Mlawi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Manejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imeeleza kuwa uhamisho huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa pamoja na shughuli nyingine za Unaibu Katibu Mkuu, Bi. Suzan Paul Mlawi, atashughulikia eneo la Utawala Bora.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria iliyoachwa wazi, haitajazwa kwa sasa.

Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
01 Februari, 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment