Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa
Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa
Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi
Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea
Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi Mteule
wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya
Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa
Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Misri
hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya
Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) Jean Pierre Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa
Afrika Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu
wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na IKULU
…………………………………………………………………………………………………….
Uingereza Imempongeza Rais Wa
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Kwa Jitihada
Zinazofanywa Na Serikali Yake Katika Ukusanyaji Wa Mapato Na Kukabiliana
Na Vitendo Vya Rushwa.
Akizungumza Baada Ya Kukutana Na
Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo,Balozi Huyo Mh Dianna
Melrose Amesema Juhudi Za Mapambano Dhidi Ya Ufisadi Pamoja Na Kubana
Matumizi Na Ubadhirifu Wa Mali Za Umma Kunakotekelezwa Kwa Vitendo Na
Serikali Ya Awamu Ya Tano Ni Mfano Wa Kuigwa.
Balozi Melrose Amesema Waziri
Mkuu Wa Nchi Ya Uingereza Bw. David Cmeroon Amevutiwa Na Utendaji Kazi
Wa Rais Magufuli Na Kusisitiza Kwamba Nchi Hiyo Itaendeleza Ushirikiano
Wa Karibu Uliopo Kati Ya Uingereza Na Tanzania Katika Nyanja Mbalimbali
Za Maendeleo………………….Mh Dianna Melrose Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini
Kabla Ya Kukutana Na Balozi Wa
Uingereza Hapa Nchini Rais Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na
Balozi Wa Afrika Ya Kusini Hapa Nchini Mh Thamsanqa Mseleku,Na Balozi Wa
Misri Hapa Nchini Mh Mohamed Yasser El Shawaf Ambao Amewahakikishia
Kuwa Serikali Yake Ya Awamu Ya Tano Itaendeleza Ushirikiano Mzuri Uliopo
Kati Yake Na Nchi Hizo Hususani Katika Kukuza Biashara Na Kuwanufaisha
Wananchi Wa Pande Zote.
Katika Hatua Nyingine Rais Magufuli Amepokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wawili.
Mabalozi Waliokabidhi Hati Zao Za
Utambulisho Ikulu Jijini Dar Es Salaam Ni Mh Jean Pierre Mutamba
Tshampanga Wa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Mh Theresia Samaria Wa
Namibia.
Rais Magufuli Amewaeleza Mabalozi
Hao Kuwa Tanzania Itaendelea kushirikiana Na Nchi Hizo Katika Nyanja
Mbalimbali Hususani Katika Uchumi.
Wakati Huo Huo Rais Wa Jamhuri Ya
Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Amekutana Na Kufanya
Mazungumzo Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
Ikulu Jijini Dar Es Salaam.


0 comments :
Post a Comment