Mkazi
wa Sitakishari Dar es Salaam, Christina Thomas (28), amekataa
kudhaminiwa ili arudi rumande na msichana wake wa kazi ambaye alishindwa
masharti ya dhamana.
Christina
jana alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumpiga
mtoto wake wa miaka miwili na kumsababishia majeraha makubwa, kuzimia na
kushindwa kumpeleka hospitalini.
Mwendesha
Mashitaka Hilda Kato, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Ritha Tarimo kwamba mshitakiwa siku isiyofahamika Januari, alimpiga kwa
fimbo mtoto huyo na kumsababishia majeraha.
Kato
alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa huyo ambaye ni mama mzazi
wa mtoto huyo na msichana wake wa kazi, Blanka Benjamin kwa uzembe
walimwacha mtoto huyo bila kumpeleka hospitali huku akiwa na hali mbaya
ambayo ilisababishwa na mama mzazi.
Baada
ya kusomewa mashitaka, mama huyo alijibu kuwa hakumbuki, huku
mshitakiwa wa pili ambaye ni msichana wa kazi akikana mashitaka yake.
Mwendesha
Mashitaka alimwambia Hakimu Tarimo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika, lakini dhamana yao iko wazi kama watakidhi masharti.
Hakimu
alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa
kuaminika mmoja akiwa mtumishi kwenye taasisi inayofahamika na kusaini
dhamana ya Sh 800,000 kila mmoja.
Baada
ya kusomewa masharti hayo ya dhamana mshitakiwa namba moja alikidhi
masharti ya dhamana huku wa pili akishindwa kutokana na wadhamini
kuchelewa.
Hata
hivyo, mshtakiwa huyo wa kwanza ambaye ni mama wa mtoto alisema hawezi
kuwa nje kwa dhamana akimwacha mshitakiwa wa pili rumande hivyo kumwomba
hakimu warudi wote ndani hadi kesho watakapotimiza masharti ya dhamana
pamoja.
Hakimu
alimwambia mshitakiwa huyo kwamba kwa sababu yeye ana mtoto mdogo hivyo
angeweza kutoka na kumwacha mshitakiwa wa pili na kesho (leo) angepata
dhamana, lakini akasema mtoto wake ataondoka na baba yake, na yeye
atarudi rumande hadi watakapopata dhamana wote wawili.
0 comments :
Post a Comment