UN
Clubs Tanzania Network kanda ya Dar es Salaam wakishirikiana na Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako wametoa msaada kwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha
Kurasini kwenye siku ya wapendanao ili kuonesha upendo mkubwa kwa
watoto hao.Vijana
hao wa UN Club Tanzania Network wanafanya kazi siku ya wapendanao nchi
nzima za kusaidia jamii na vijana wa jijini Dar es salaam wameungana na
watoto wa kituo cha Kurasini kwa kutoa msaada na wanafunzi hao wametoka
katika shule za sekondari za Zanaki, Azania, Benjamin na Jangwani.
Akizungumzia msaada huo, Afisa
Ustawi wa Jamii katika kituo hicho. Jack Omary aliwashukuru kwa
kuwatembelea siku ya wapendanao maana kuna watu wengine wanaitumia siku
ya wapendanao kwenye starehe na hata kutumia pesa bila kuangalia kuna
watu wanahitaji msaada.
Nae Stella kutoka UN Clubs Tanzania amesema lengo la kuja katika kituo cha watoto yatima cha Kurasini nikujumuika na hao watoto ambao hawana wazazi na pia watoto wenye shida mbalimbali.
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akiwakabidhi misaada watoto wa Kituo cha Kurasini, katikati ni mtoto Aboubakary Seif ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wenzake.

Alisema
inabidi kuwakumbuka hasa kwenye siku kama za wapendanao kwani kuna watu
wanatumia pesa nyingi kwenye starehe kuliko kutoa misaada kwa watoto
wenye mahitaji maalumu hasa wazee,walemavu na hata watoto yatima.Mtoto
Aboubakary Seif anayelelewa katika kituo hicho cha Kurasini
amewashukuru UN Clubs Tanzania Network Pamoja na Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kwa
kuwaona kama watu katika jamii wanakubalika hasa kwenye siku ya
wapendanao.
Amesema
wao wamesijsikia furaha kutembelewa na vijana wenzao na kuwapa moyo
hasa kwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.Pia
aliwaomba watu wengine wenye uwezo waje kutoa msaada maana matatizo ni
mengi na matatizo hayo yatatatuliwa kwa misaada ya wadau mbalimbali.
Picha ya pamoja.

0 comments :
Post a Comment