Baada ya jana, jumatatu kuwepo kwa taarifa kuwa Manchester United ipo tayari kulipa kiasi cha Pauni Milioni 60 kwa ajili ya kupata saini ya staa wa Gabon na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Pierre-Emerick Aubameyang, leo imetoka stori nyingine kuhusu usajili wa mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mirror umeripoti kuwa Manchester United ipo tayari kumlipa Aubameyang mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki pindi atakatua kwenye klabu hiyo ya Uingereza.
Mtandao huo umeripoti kuwa uhamisho wa Aubameyang unauwezekano mkubwa kukamilika baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa wawakilishi wa Aubameyang wameshakutana na viongozi wa Man United ili kujadili uhamisho huo.
Aubameyang, 26 kwa msimu wa 2015/2016 ameshaifungia klabu yake ya Dortmund magoli 30 na hivyo kuzivutia klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwepo Arsenal ili kupata saini ya mchezaji huyo bora Afrika, 2015.