UNAMJUA RAIS MPYA WA SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI (FIFA) ALIESHINDA NAFASI HIYO USIKU WA IJUMAA HII? HUYU HAPA

Nkupamah media:
Gianni Infantino
Kiti cha urais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA) kimepata rais mpya baada ya miaka 18 kushikiliwa na Sepp Blatter baada ya kufanyika uchaguzi usiku wa Ijumaa na Gianni Infantino kufanikiwa kushinda nafasi hiyo.
Infantino amefanikiwa kushinda nafasi hiyo ya juu FIFA baada ya kuwashinda wapinzani wake ambapo amepata kura 115, Sheikh Salam 88, Prince Ali al-Hussein 4 na Jerome Champagne akikosa kura kabisa.

Rais mpya wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino
Baada ya matokeo hayo kutangazwa Infantino ameonekana mtu mwenye furaha kwa kupata ushindi huo na kusema kuwa “Wapendwa, siwezi kusema jinsi ninavyojisikia kwa wakati huu” alisema na kuongeza.
“Niliwaambia ninakwenda safarini, safari ya kipekee, safari ambayo itanifanya nikutane na watu tofautitofauti wengi wao wakiwa wapenda soka, wanaoishi katika soka, wanaopumua katika soka kila siku na watu wengi ambao wanastahili heshima hii kutoka FIFA”(P.T)
Share on Google Plus

About Mng'atuzi blog

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment