Nkupamah Media:
Ray Kigosi
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Ray alisema huu ni wakati kwa wadau wa filamu pamoja na mashabiki kusupport wasanii waliopo kwa nunua kazi zao.
“Mimi nataka mashabiki wa filamu wajue hii tasnia inaendeshwa na wao, sisi wasanii tunategemea support yao kwa kununua kazi zetu. Mimi binafsi naukubali mchango wa Kanumba lakini ufike wakati tujue ya Kanumba yalishapita, tuwaandae akina Kanumba wengine, na wanaosema tasnia ya filamu imekufa baada ya Kanumba kufariki sio kweli na wapuuzwe.” Alisema Ray.
Aliongeza, “Mimi naamini tuna wasanii wengi wenye vipaji ambao tukiwasupport tutafika mbali zaidi. Mbona kwenye muziki leo kuna Diamond, lakini hapo nyuma kulikuwa na akina MB Dog, Matonya, TID na wengine wengi. Mimi naamini hata Diamond wakati wake ukipita watakuja wengine wakali. Kwahiyo nawaambia mashabiki wa filamu tuna wasanii wengi bado wanafanya vizuri, kinachotakiwa ni kuwasupport alafu tuone kama watashindwa.”.
Aidha, Ray amewakata mashabiki wa filamu kuisubiria filamu yake mpya ‘Tajiri Mfupi’ ambayo inatarajia kutoka hivi karibuni.
0 comments :
Post a Comment