Nkupamah media:
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo anatarajia kuanza ziara ya siku 14
katika mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema Waziri Mkuu anayetarajiwa
kufika Mwanza saa nane mchana, atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma,
Geita na Kagera.
“Ingawa hakuna ratiba ya kutembelea eneo lolote
mkoani Mwanza, tumejipanga kila idara endapo atafanya ziara ya
kushtukiza, tuko tayari,” alisema.
Wakati huohuo; Mulongo
alisema mke wa Rais, Janet Magufuli anatarajiwa kutembelea Kituo cha
Kulea Wazee Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi.
“Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka,” alisema Mulongo.
0 comments :
Post a Comment