Ligi ya Mabingwa ya barani Ulaya iliendelea jana kwa michezo ya kwanza ya hatua ya 16 bora ambapo michezo miwili ilichezwa. Benfica ya Ureno iliikaribisha Zenit St. Petersburg na mchezo wa pili ukiwa ni Paris Saint-German iliyokuwa mwenyeji wa Chelsea ya Uingereza.
Mchezo wa PSG na Chelsea ulimalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja, magoli yakifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 19 na Edson Cavani dakika ya 78 na goli la Chelsea likifungwa na John Obi Mikel.

Mchezo mwingine ulimalizika kwa wenyeji Benfica kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, goli likifungwa na Jonas Oliveira katika dakika ya 90+1.