Nkupamah media:
![]() |
Bw Polepole akimpongeza mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela wakati wa kongamano la shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la wana CCM mkoa wa Iringa jana |

.Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akiwa amembeba mmoja kati ya watoto wakazi wa kijiji cha Mboliboli tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa ambao wamekumbwa na mafuriko ambayo maji yake yana vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa zaidi ya siku nne sasa baadhi yao bado wanaishi juu ya vichuguu
Mkuu wa wilaya ya Iringa akizungunza na wananchi waliookolewa katika mafuriko Pawaga
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na wanafuzi wa vyuo vikuu mkoa wa Iringa wakati wa kongamano la jana kushoto ni Bw Polepole na kulia na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw salim Asas na katibu wa shirikisho hilo Bi mariam Fundi
Na MatukiodaimaBlog
ALIYEKUWA mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba BW Humphrey Pole pole amempongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kujitoa kunusuru uhai wa wananchi wa kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga ambao wamekubwa na mafuriko yenye vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kuwa mkuu huyo wa wilaya ni hazina kubwa ya Taifa na kumwomba Rais Dr John Magufuli kumkumbuka katika ufalme wake.
Huku akidai kuwa kazi inayoendelea kufanywa na rais Dr Magufuli ya kutumbua majipu wapo ambao wanaumizwa zaidi kutokana na kupoteza imani ya kuendelea kuishi maisha ya kula bata kila uchwao.
Bw Polepole ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM na siku 100 za Rais Dr Magufuli lililoandaliwa na shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa lililofanyika jana mjini hapa alisema kuwa amepata kushuhudia kupitia vyombo vya habari mbali mbali jinsi ambavyo mkuu huyo wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela anavyojitolea kuokoa maisha ya wananchi wake jambo ambalo kwa viongozi wengine ni vigumu kufanya hivyo.
Alisema kuwa kati ya wakuu wa wilaya ambao wamekuwa wakiitambua kazi yao kwa wananchi na wananchi wakiona bila tatizo kazi inayofanywa na kiongozi wao ni pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ambae ushujaa na uzalendo wake kwa wananchi wake ni mkubwa na mfano wa kuigwa na viongozi wengine katika kuwatumikia wananchi.
" Tanzania ya Rais Dr Magufuli itapiga hatua kubwa zaidi ya leo tunapotathimini siku 100 za utawala wake iwapo watendaji wote watatambua wajibu wao kwa wananchi wao badala ya kutangulia maslahi yao kwa taifa yao....nimependezwa sana na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wananchi ambao mkuu huyu wa wilaya kakangu Richard Kasesela anaonyesha ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kwa moyo .....nimeona katika mitandao ya kijamii mkuu huyu wa wilaya akiogelea katika maji kuokoa maisha ya wananchi wake ambao wamekubwa na mafuriko tena maji yenye vimelea vya kipindupindu ....ni nani angeweza kuhatarisha maisha yake hivi zaidi ya kutuma waliopo chini yake kufanya kazi kwa niaba yake" alihoji Bw polepole.
Huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzidi kutumika vema kwa ajili ya wananchi wake na kuomba iwapo inawezekana Rais Dr Magufuli kwenye utumbuaji wake wa majipu kwa wakuu wa wilaya na mikoa kuangalia wakuu wa wilaya wasio tambua wajibu wao ambao wapo kwa ajili ya faida yao na kuwaacha ama kuwapandisha vyeo zaidi wale ambao wamekuwa wakifanya vizuri.
" Simpigii debe Kasesela ila naongea ukweli ulio wazi kwa kila mmoja wenu hasa watu wa Iringa ambao mmekuwa nae ....binafsi nimevutiwa na utendaji wake mzuri nampongeza sana".
Hata hivyo Bw Polepole alisema kuwa kazi inayofanywa na Rais Dr Magufuli ya kutumbua majipu ni kazi ya nzuri kwa watanzania swapenda uzalendo ila wapo wanaoumia kwa ndugu zao ama wenyewe kutokuwa na uhakika wa kuendelea kufanya anasa za matumizi ya pesa ama kupata mkate wa kila siku.
" Hii ni kazi nzuri sana na inapaswa kuendelea kwa nguvu zote ...ila tuwe wakweli hapa wengi tunashangilia kuona majipu ambayo si ndugu yanatumbuliwa hivi inakuwaje kama zamu ya kutumbua jipu ingekuhusu wewe ama mzazi wako .....bila shaka ungeona zoezi hili ni baya zaidi lakini kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ya wote lazima tuwe wapole tuache kila jipu litumbuliwe kwa afya yako ".
Aidha alisema utendaji mzuri wa Dr Magufuli na serikali yake ya CCM umepelekea wapinzani nchini kukosa hoja ya kuzungumza na kuendelea kuokoteza maneno ya kuongea ili mradi waonekane wameongea jambo lakini kimoyo moyo wanapongeza kazi nzuri ya serikali ya CCM chini ya rais Dr Magufuli.
Pia alipongeza imani kubwa ya wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kutoka vyuo vikuu vya Iringa ambao wamehama vyama hivyo na kujiunga na CCM baada ya kupendezwa na utendaji mzuri wa Rais Dr Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM na kuwataka wengine kuzidi kurudi CCM kwani wapende wasipende kasi ya rais Dr Magufuli ni kubwa tofauti na walivyotegemea.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela pamoja na kumpongeza Bw polepole kwa kuendelea kuelimisha umma kupitia vyombo mbali mbali vya habari juu sera nzuri za CCM na kutambua kazi anayoifanya yeye kama mkuu wa wilaya ,bado alitaka wasomi nchini kutokubali kupandikizwa siasa chafu za kulalamika na kutuhumu kila uchwao na badala yake wao kuwa msaada kwa umma.
Alisema wapo baadhi ya wana siasa wanatumia wasomi kuhadaha umma kwa faida yao badala ya kuelimisha umma kwa kueleza ukweli nini CCM imefanya kwa miaka yake 39.
" wapo baadhi ya wanasiasa wao kazi kwao ni kusema ovyo ovyo serikali ya CCM na wengine wapo hadi Iringa ambao wao bila kutukana ama kuisema vibaya serikali ya CCM kwao siku haijapita .... binafsi sitanyamaza kuona mwana siasa ama mtu yeyote akimsema ovyoovyo Rais wangu Dr John Pombe Magufuli kama akiongea mbele yangu ngumi moja mbili nitampa na akiongeza mbali ya mimi kama katika vyombo vya habari nitamjibu haraka.....siwezi hata siku moja kuvumilia mtu msema ovyo heri hata huu ukuu wa wilaya nipoteze kwa kuitetea serikali yangu ya CCM"
0 comments :
Post a Comment