18 KUIVAA SIMBA SC

Nkupamah media:

????????????????????????????????????
Kocha Mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri ametangaza majina ya nyota 18 watakaoivaa Simba Sports Club  kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania bara uliopangwa kuchezwa  jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mapema leo Phiri ameuambia  mtandao huu kuwa anatua jijini Dar na kikosi cha nyota hao ambao aliwaandaa maalumu kwa mchezo huo wa mwishoni mwa juma akiwa na imani kubwa kuwa wataiwezesha City kuibuka na ushindi kutokana na  kuiva  vizuri kimazoezi na mafunzo waliyoyapata katika wiki nzima ya maandalizianya .
“Nina imani nao kuwa,wamefanya vizuri sana kwenye mazoezi ya wiki hii, sina shaka na wao kutupatia matokeo kwa sababu wako sawa tayari kwa mchezo,tutacheza kwenye mfumo mpya ambao haujawahi kuonekana tukicheza, hii ni kwa sababu tumedhamiria kupata ushindi kama ambavyo timu imekuwa ikifanya kila inapokutana na Simba”, alisema.
Miongoni mwa nyota walio kwenye orodha ya kuivaa Simba siku hiyo ya jumapili ni pamoja na mlinzi Hassan Mwasapili, mlinda lango Haningtony Kalyesubula pia wamo Temi Felix, Haruna Shamte,Yohana Moriss,Kenny Ally na wakali wengine 12 ambao wamepewa majukumu kadhaa kuhakikisha  City inaandikisha pointi tatu muhimu mbele ya timu hiyo ya Msimbazi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment