Elisabet
alipokuwa mdogo wa miaka miwili na nusu alichukuliwa na watu wawili
raia wa Sweden ambao walimchukua kwenda kuishi nae kutoka katika kituo
kilichokuwa kikimlea.
Alieleza
kuwa wakati akiwa Sweden alitaka kwenda kumtafuta mama yake lakini
walezi wake walimtaka aendelee na maisha yake bila kumtafuta lakini
alikwenda mwaka 1998 kumtafuta lakini ilikuwa sio rahisi kumpata na
ndipo mwaka 2014 alipoamua kuwasiliana na Shirika linalopinga vitendo
vya wizi wa watoto (ACT).
Aliongeza
kuwa Agosti, 8 mwaka jana alipokea taarifa za kupatikana kwa mama yake
kutoka ACT na kumtumia baadhi ya picha za mama yake.
“Siwezi
kuelezea hisia zangu, ni mtu ambaye nilikuwa naye mbali kwa maisha
yangu yote alafu namuona kwenye picha, ulikuwa kama muujiza, ni muujiza
mkubwa,” alisema Elisabet.
Chanzo: BBC
0 comments :
Post a Comment