Chama
cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimemuomba Waziri Ofisi ya
Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na
Utawala Bora, George Simbachawene kuwawajibisha Wakurugenzi wa Manispaa
ya Ilala na Kinondoni kwa kile walichodai ni kuvuruga uchaguzi wa Meya
wa Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yalizungumzwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM Mkoa wa Dar e Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ wakati akizungumza na
waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na sintofahamu hadi sasa
kuhusiana na uchaguzi huo kutokana na woga wa wakurugenzi hao ambao
wameshindwa kujiamini.
“Wakurugenzi hawa ndiyo chanzo cha vurugu katika uchaguzi huu wa meya
tumewaomba wakurugenzi hawa watoe tamko na tafsri sahihi ya ushiriki kwa
wajumbe wenye sifa ili kuacha kuupotosha umma juu ya uchaguzi huu,”
alisema Gadafi.
Gadafi alisema kuwa wakurugenzi hao kwa makusudi na huku wakifahamu wanakiuka sheria waliruhusu baadhi ya maswahiba wao kutoka chama cha upinzani ( Ukawa) ambao walitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuingia kwenye uchaguzi uliovurugika.
Gadafi alisema mwanachama yeyote wa CCM anaruhusiwa kufanya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kupingwa kama taratibu unavyoelekeza.

Alisema hizi kauli zinazotolewa kuwa haiwezekani wajumbe wakatoka nje
ya Dar es Salaam na kupiga kula eneo lingine hazina ukweli wowote kwani
siku za nyuma ziliwahi kufanyika kwa vyama vingine lakini hakukuwa na
kulalamika.
Aidha katika hatua nyingine Simba amesema Meya wa Ukawa walioshinda
katika Manispaa za Kinondoni na Ilala wanatakiwa watambue kuwa
Halmshauri hizo hazitaendeshwa kwa ilani ya chama chao bali ni ilani ya
Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo
inaongozwa na chama. 

0 comments :
Post a Comment