Mshambuliaji
wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale amefanikiwa kuwa mmoja wa
wachezaji ambao wameingia katika historia ya Ligi Kuu ya Hispania (La
Liga) baada ya kuisaidia timu yake ya Madrid kuibuka na ushindi wa goli 4
– 0 kwa bila dhidi ya Sevilla.
Bale
ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka British (Uingereza,
Wales, Ireland na Scotland) kufunga magoli 43 katika ligi hiyo akiwa
amecheza michezo 76 pekee.
Awali
kabla ya Bale, rekodi ilikuwa ikishikiliwa na Gary Lineker ambaye
alifunga magoli 42 katika michezo 103 akiitumikia Barcelona mwaka
1986-1989.


0 comments :
Post a Comment