Baada
ya kuwepo kwa maneno mbalimbali ambayo yalikuwa yakizunguzwa hatimaye
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amezungumzia uchaguzi mkuu wa Meya wa Dar
es Salaam.
Rais
Magufuli amezungumzia uchaguzi huo wakati alipokuwa akitekeleza agizo
la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda la kutaka kuhakikiwa kwa silaha
zote zinazomilikiwa na wananchi ambapo yeye amehakikiwa silaha
anazomiliki ambazo ni Shortgun na Pisto.
Ili
kufanyika kwa uchaguzi huo Dkt. Magufuli amezitaka pande zote ambazo
zinagombea kiti cha umeya wa jiji la Dar es Salaam, kukamilisha mchakato
wa kumpata meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho Machi, 22
badala ya kuendelea kurumbana.
Dkt.
Magufuli amesema kuwa upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya
uchaguzi huo, ili meya apatikane na jiji liweze kuendelea na mipango
yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.
“Mahali
tunapostahili kushinda kama tunashinda tushinde kweli, lakini mahali
tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndiyo demokrasia ya
kweli,” amesema Dkt. Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli amezungumzia zoezi la uhakiki wa silaha na kumpongeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Jeshi la Polisi kwa kuanzisha zoezi
hilo na kuwataka wamiliki wa silaha nchi nchi nzima kuhakikisha
wanahakiki silaha wanazomiliki.
Pia
amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi ili kukabiliana na watu
wanaojihusisha na vitendo vya uharifu ili kutokomeza kabisa vitendo
hivyo.
“Ni
aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang’anywa silaha, ni aibu
na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang’anye silaha na wewe una
silaha,” amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Simon Sirro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono zoezi
hilo na amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha zoezi hilo
linafanyika kwa uhakika.


0 comments :
Post a Comment