LUKUVI APOKEA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO IRINGA.

Nkupamah media

vi2
Mhe. William Lukuvi akipokea msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao Makuu  ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu TGGA.
vi3
Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa.
vi1
Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe. Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni  Chakula, Nguo , viatu na Madaftari.
vi4
Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.
 ………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155, Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.
Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment