Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni
Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.
Katika barua hiyo, Malinzi
amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa
niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea
kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia
kila la kheri na mafanikiko mema.
0 comments :
Post a Comment