Tayari maandalizi ya tamsha la Upendo Music Festival ambaloo linatarajia kufanyika Jumapili ya Pasaka kesho Machi 27.2016 yamekamilika kwa asilimia mia moja.
Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited tayari imeweka wazi baadhi ya vikundi na wasanii washiriki wa tamasha hilo.
Watakao muimbia Mungu katika tamasha hilo baadhi ya Wasanii hao wenye kalama na upeo mkubwa katika kumuimbia Mungu ni pamoja na: Angel Bernard, Emanuel Mbasha, Lynga George, Upendo Kihaile, Sarah Shilla, Faraja Ntaboba.
Pia wapo: Edson Mwasabwite, Angel Magoti, Abeid Ngosso, Ambwene Mwasongwe na Fridah Felix na wengine wengi wakiwemo Choir ya Kigogo KKKT, Gift and Beauty, Moses Saxer, Mise Ricprdias, The Joshua Generation, Glorious Worship Team, The Voice, Uinjilist Choir Kimara, Doxers Praise Team, Calvary Band, The Jordan, The Next level, Chang’ombe Vijana Choir, Uinjilist Kijitonyaama, Tumaini Shangilieni Choir na wengineo.
Katika tamasha hilo hiyo siku ya Jumapili ya PASAKA, katika viwanja vya LEADERS CLUB, Kinondoni, linatarajia kuanza majira ya asubuhi ya nne ( 4:00) Hadi Saa 10:00 Usiku. Pia litajumuisha na Bonanza la Michezo, Michezo ya Watoto na Uuzaji wa Biashara mbali mbali huku kiingilio kawaida ni Tsh. 5,000 na kwa viti maalum ni Tsh.10,000 huku kwa Watoto ni Tsh. 2,000.
“Music 100% Live, Njoo tumuimbie Mungu”.. Ulinzi na Usalama ni wa hali ya juu nyoote munakaribiswa.
Maandalizi ya jukwaa litakalofanyika tamasha hilo la Upendo linavyoonekana kwa sasa majira ua mchana. Jukwaa hilo limefungwa tokea jana.
Jukwaa hilo linavyoonekana majira ya usiku..
Baadhi wasanii washiriki watakaokuwapo kwenye tamsha hilo la Upendo hiyo kesho.

0 comments :
Post a Comment