Nkupamah media:
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea
na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo, wakati
alipofanya nao mkutano kwa mara ya kwanza tanga ateuliwe kushika wadhifa
huo. Kushoto ni Mwanasheria wa TCAA, Patrice Chegani.
Baadhi ya wafanyaakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA, wakimsikilaza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Hamza Johari hayupo pichani, wakati alipokutana nao kwa mazungumuo ya utendaji kazi leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Hamza Johari,
amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kujiangalia pale wanapoona
waliteleza na kubadilika kwa kufanya mabadiliko na kuachana na tamaduni
walizoziea hapo awali.
Mkurugenzi
Johari aliyasema hayo leo alipokuwa katika kikao chake cha kwanza
kilichafanyikia TCAA Makao Makuu na kuhusisha wafanyakazi wa TCAA wa
Makao makuu, kituo cha uwanja wa ndege wa JNIA, chuo cha usafiri wa Anga
(CATC) na Karakana ya TCAA Chang’ombe baada ya kuteuliwa kushika
wadhifa huo hivi karibuni, na kuongeza kuwa kila mtu au kila jamii ina
utamaduni fulani, tatizo ni tafsiri au namna tamaduni hiyo ilivyo
inaweza kuwa nzuri ama mbaya.
Bw.
Johari ameongeza pia kuwa yeye anawaona wafanyakazi wote wa TCAA kama
timu moja ya ushindi na anaamini kwa kufanya kazi kwa kushirikiana basi
TCAA itapiga hatua na ikitokea kinyume chake TCAA Itakwama .
Bw.Hamza
pia amesisitiza juu ya kila mmoja kutimiza wajibu wake mahala pake pa
kazi na yeye pia kama Mkurugenzi Mkuu atatimiza ya upande wake, lengo
likiwa kuipigisha TCAA hatua.
Ameongeza
pia kuwa, katika kipindi hiki cha uongozi wake atahakikisha masuala
mbali mbali ambayo ni changamoto kwa wafanyakazi wa TCAA yanaangaliwa
upya na kuboreshwa, ili waweze kuongeza Ari ya kufanya kazi.
Akitoa
salamu ya shukran kwa niaba ya wafanyakazi wa TCAA, Katibu Mkuu wa
TUGHE –TCAA Bw.Maotola Miti alimuakikishia Mkurugenzi Johari kwamba
wafanyakazi wote wa TCAA wapo nyuma yake katika kufanikisha malengo ya
TCAA kupiga hatua yanafanikiwa, na kuongeza kuwa wafanyakazi wa TCAA
wana matumaini makubwa juu yake.
0 comments :
Post a Comment