Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kazi rasmi leo Machi 16.2016 majira ya
mchana ambapo alifanya mazungumzo na wakuu wa idara na Vitengo
mbalimbali na kutoa maagizo mazito ambapo alitoa masaa 24 kwa wakuu hao
kumpa taarifa zilizopo katika maeneo yao husika zenye kuelezea
changamoto mbalimbali ili kuona wananchi wanakabiliwa na changamoto zipi
na namna atakavyoweza kuzitatua.
Makonda
aliyasema hayo wakati akizungumza na wakuu hao wa idara na vitengo
katika hafla fupi ya kukaribishwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali ya wakuu hao wa idara na
vitengo pia ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu
Tawala wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.


0 comments :
Post a Comment