Baada ya kuchelewa mazoezini na sababu yake kuwa ni amepuuzia kengele, uongozi wa klabu yake ya Wolfsburg ulimpa adhabu ya kulipa Pauni 39 kwa kila dakika aliyochelewa ambapo kwa dakika 45 ikawa ni Pauni 1,770 na pia akaambiwa afanye mazoezi peke yake.
Akizungumza na gazeti la Ujerumani la Bild, Bendtner alisema “Nilipitiwa kulala, nilipuuzia kengele, ni kosa langu”
Hilo sio kosa la kwanza la Bendtner kulifanya tangu alipowasili katika klabu hiyo kwani hata mwezi uliopita alikwenda mazoezini akitumia gari aina ya Mercedes S-Class licha ya kufahamu kuwa hawaruhusiwi kwenda mazoezini na gari za kampuni nyingine kutokana na klabu hiyo kuwa na mkataba na kampuni nyingine ya magari ya Volkswagen.