Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw.
Alvaro Rodriguez (kulia) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) wakipata maelezo
kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa shamba la muhogo huku wakiangalia
shina la muhogo mchanga kabla ya kukomaa.
Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw.
Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (kushoto)
wakiangalia sehemu ya tawi la mmea wa muhogo uliopo shambani
walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wa mihogo Wilaya ya Rufiji
jana.
MRATIBU Mkazi na Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UN), Alvaro Rodriguez
amefanya ziara ya kutembelea mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la
muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya
Rufiji Mkowa wa Pwani kuangalia namna kiwanda hicho kinavyo ongeza
thamani za zao la muhongo na kuboresha kipata cha wakulima.
Katika ziara hiyo, Bw. Alvaro
Rodriguez aliongozana na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika ambaye shirika lake limekubali
kusaidia kukiendeleza kiwanda hicho kupata mashine ya kisasa pamoja na
uwezo wa nguvu kazi kuongeza ufanisi wa kiwanda.
Akizungumza katika kiwanda hicho,
Bw. Malika alisema UNCDF imekubali kukisaidia kiwanda hicho ili kuinua
hali ya kipato cha wakulima wa zao la muhogo wa Wilaya ya Rufiji ambao
tayari walianza kuzalisha mazao hayo kwa kukitegemea kiwanda cha
‘African Starch Project’ ambacho kilisimamisha uzalishaji kutokana na
uwezo mdogo wa mashine zake.
“…UNCDF tumekubali kutoa mtaji wa
kuanzia pamoja na kuwezesha nguvu kazi ili kiwanda kiweze kujiendesha
kibiashara na kuendelea kuwanufaisha wakulima wa zao la muhogo eneo
hili…tayari wamehamasika na kilimo hiki baada ya kuletwa kwa mradi huu
sasa tunataka kuuongezea nguvu zaidi,” alisema Kiongozi na Mshauri wa
Ufundi wa Shirika la UNCDF, Malika.
Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,
Alvaro Rodriguez (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea
ofisi hizo jana. Kulia ni Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika.
Mtaalamu
wa Mawasiliano, Ushirikiano na Utafutaji Mitaji kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Jacqueline Namfua
akiwatambulisha Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Kiongozi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika
(katikati) kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape
waendeshaji wa mradi huo alisema kwa sasa wakulima zaidi ya 500 wa zao
la muhogo wameanza kunufaika na mradi huo ambao wamekuwa wakitegemea
kukiuzia kiwanda muhogo wa kuchakata jambo ambalo limekuza kipato chao.
Alisema ufadhili wa UNCDF
utakapokamilika kimtaji katika kiwanda chao zaidi ya wakulima 7000
watakuwa wakinufaika ndani ya miaka miwili, ambapo zao wanalolilima
litaitajika kwa wingi kiwandani hivyo kuboresha hali za kiuchumi kwa
jamii, lakini lengo kwa hapo baadaye ni kuhakikisha wakulima 10000
wananufaika na shughuli nzima za mradi huo wa kiwanda.
Aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya
vijiji 20 wilayani Rufiji vinavyozunguka kiwanda hiko wananchi wake wapo
tayari kufanya biashara ya kilimo kukipatia kiwanda muhogo wa
kuchakata, ambapo watakuwa wakishiriki kuwawezesha wananchi katika
vikundi ili waweze kufanya uzalishaji wa kutosha kiwandani.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima
wakiwemo akinamama waliozungumza katika ziara hiyo wamelishukuru
shirika la UNCDF kwa kufadhili kiwanda hicho kwani tendo hilo
limewahakikishia upatikanaji wa soko la uhakika kwa zao la muhogo,
ambalo hapo awali lilikuwa likilegalega kutokana na kupoteza kiasi
kikubwa cha mabaki ya zao hilo.
UNCDF inategemea kutumia
takribani shilingi milioni 400 kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda cha
kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo eneo hilo.
Ziara ya viongozi hao ambao waliambatana na wajumbe wa manamawasiliano
wa mashirika ya umoja wa mataifa iliwafikisha katika Halmashauri ya
Wilaya ya Rufiji na kufanya mazungumzo na viongozi wa halmashauri kujua
changamoto anuai za kijamii.
Ujumbe
huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na
Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw.
Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha
muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda
wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezio.

Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape
(kushoto) akielezea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kutoka kulia
wanaomsikiliza ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini
Tanzania, Magnus Minja, Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika na Mratibu Mkazi na Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa
kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna
kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN
nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia).
Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania,
Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF.
Ujumbe
huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la
muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS
African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).
Ujumbe
huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la
muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS
African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).
Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape
akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho (hawapo pichani) namna
bidhaa aina ya Starch na unga wa muogo unavyozalishwa mara baada ya
kuchakata muhogo.
Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa
kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna
kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN
nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia).
Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania,
Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF.
Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw.
Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika
na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’
kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana
walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima
wa muhogo eneo hilo.
Mmoja
wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea
wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini
Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.
Mratibu
Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,
Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na baadhi ya wakulima
wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch
Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana
walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima
wa muhogo eneo hilo.
Kiongozi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter
Malika akizungumza na baadhi ya wanahabari na ujumbe wa wanamawasiliano
(hawapo pichani) baada ya ziara ya kukitembelea kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo eneo la Bungu Wilaya ya
Rufiji jana.
Mmoja
wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea
wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini
Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.
Kutoka
kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,
Hoyce Temu, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,
Bw. Rodriguez pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika wakitembelea moja ya mashamba
ya zao la muhogo wilayani Rufiji jana.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

0 comments :
Post a Comment