Muhimbili yapokea majeruhi wa ajali iliyotokea Bagamoyo


aja1
Moja ya gari lililopata ajali katika msafara wa Waziri Suleiman Jafo.
……………………………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea majeruhi watano wa ajali ambayo imetokea katika eneo la Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani iliyohusisha wafanyakazi wa Halmshauri ya Bagamoyo wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Bunge, Utawala na Tamisemi kama ilivyoripotiwa na mitandao mbalimbali ya  kijamii.
Pia, Hospitali imepokea mwili wa mtu mmoja ambaye amefariki dunia wakati akiletwa hospitali hapa aliyefahamika kuwa ni Juliana Masaga ambaye alikuwa mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Majeruhi waliopokelewa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo, Ibrahim Matovu, Julius Mwanganda ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, George Mashauri Mweka Hazina, Doroth Njitile, mratibu wa TASAF na Tanwira Khalid ambaye ni raia.
Kati ya majeruhi hao, Doroth amefanyiwa upasuaji baada ya kuumia kifua, sehemu za miguu na tumbo. Majeruhi wengine wanne wameumia sehemu za miguu na kuhamishiwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefika kuwajulia hali majeruhi kwenye hospitali hiyo leo. Hata hivyo kutokana na maadili ya kutoa huduma kwa wagonjwa walioko eneo la dharura hatukupiga picha  wakati wakihudumiwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment